Tangazo la Kuitwa Kazini Kada ya Afya Tamisemi

Popular

Full Details

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS

Kumb. Na. CD. 162/355/01/120 20/12/2017

TANGAZO LA KUITWA KAZINI
OR TAMISEMI inapenda kuwataarifu walioomba kazi kuanzia tarehe
25/07/2017 hadi tarehe 11/08/2017 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya
kazi awamu ya III umekamilika.
Waombaji wote waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuzingatia
maelekezo yafuatayo:-

i) Kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda wa siku
kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili. Aidha waombaji
watakaoshindwa kuripoti kwenye vituo vya kazi ndani ya siku kumi na
nne (14) nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine haraka
iwezekanavyo.

ii) Kuwasilisha kwa waajiri wao vyeti halisi (Originals Certificates) vya
masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya kuhakikiwa
na waajiri kabla ya kupewa barua za ajira.

iii) Hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi, watakaoshindwa
kuripoti katika muda uliopangwa, nafasi zao zitajazwa na waombaji
wengine haraka iwezekanavyo.

Orodha ya majina ya waombaji waliopangiwa vituo vya kazi inapatikana
kupitia tovuti ya OR TAMISEMI www.tamisemi.go.tz  au
http://blog.tamisemi.go.tz 

Kwa waombaji wote ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili,
watambue kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara
nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Limetolewa na:
Rebecca Kwandu
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
OR – TAMISEMI

Ad details

Ad ID : 7997
12158 Views

Advertiser details

Ajira Zetu (1513)
Contact Advertiser Share

Phone number

Sorry, you need to register or login first.

Tangazo la  Kuitwa Kazini Kada ya Afya Tamisemi

Contact form

Sorry, you need to register or login first.

Add to favorites

Sorry, you need to register or login first.