Tangazo la Kuitwa Kazini Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari Awamu ya Kwanza 2017/18

Popular

Full Details


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS - TAMISEMI

 

OR-TAMISEMI inapenda kuutarifu Umma kuhusu ajira
mpya kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari. Majina
ya Walimu haya yanatokana na Tangazo la Serikali la kuziba
nafasi zilizoachwa wazi na Walimu katika Shule za Msingi na
Sekondari waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi mapema
mwaka huu na hivyo kuondolewa kwenye Utumishi wa
Umma.

Baada ya uhakiki wa maombi ya Walimu yaliyotumwa
Serikalini, jumla ya Walimu 3,033 wamechaguliwa na
kupangiwa vituo vya kazi. Kati yao, Walimu 266 ni wa
Sekondari na Walimu 2,767 ni shule za msingi. Walimu hao
watatakiwa kuripoti katika Ofisi za Wakurugenzi wa
Halmashauri zilipo shule walizopangiwa na kisha
watakwenda kuripoti kwenye Shule hizo. Walimu hao
wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 27 Desemba, 2017 hadi
tarehe 07 Januari, 2018 wakiwa na mahitaji yafuatayo:-

(i) Vyeti halisi vya taaluma vya Kidato cha Nne na Kidato
cha Sita;

(ii) Cheti halisi cha kitaalamu cha kuhitimu mafunzo ya
Ualimu kwa ngazi husika; na
(iii) Cheti cha kuzaliwa.
Aidha, napenda kuwaelekeza walimu waajiriwa wapya waliopangiwa
vituo vya kazi kuwa:

i. Vituo vyao vya kazi ni Shule za Msingi kwa walimu
waliopangiwa kufundisha Elimu ya Msingi na Shule za
Sekondari kwa walimu waliopangiwa kufundisha
Elimu ya Sekondari na sio Makao Makuu ya
Halmashauri.

ii. Mwalimu yeyote atakayebainika kuchukua posho ya
kujikimu na baadaye kuondoka/kutoroka kwenye kituo
chake cha kazi alichopangiwa atachukuliwa hatua kwa
mujibu wa Sheria.

iii. Kila mwalimu amepangiwa kwenye shule ambayo ama
haina walimu wa somo husika kabisa au kuna upungufu
mkubwa shuleni hapo. Hivyo, waajiriwa wapya
hawatahamishwa kutoka shule moja kwenda shule
nyingine ndani au nje ya Halmashauri au Mkoa bila
ridhaa ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI.

Wakurugenzi wa Halmashauri wanatakiwa kuwapokea Walimu
wapya kwa kuzingatia taratibu na kanuni zote za Utumishi wa Umma,
ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya kuripoti kwao. Taarifa ya kuripoti
waajiriwa wapya itumwe Ofisi ya Rais- TAMISEMI ifikapo au kabla ya
tarehe 10 Januari, 2018.
Orodha ya majina ya Walimu waliopangiwa vituo vya kazi
inapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI ya
www.tamisemi.go.tz 

Imetolewa na:
KATIBU MKUU
OFISI YA RAIS - TAMISEMI

Ad details

Ad ID : 7996
4332 Views

Advertiser details

Ajira Zetu (1513)
Contact Advertiser Share

Phone number

Sorry, you need to register or login first.

Tangazo la Kuitwa Kazini Walimu wa  Shule za Msingi na Sekondari Awamu ya Kwanza   2017/18

Contact form

Sorry, you need to register or login first.

Add to favorites

Sorry, you need to register or login first.